8 Desemba 2018 - 19:48
Ufaransa inapaswa kuwekewa vikwazo

Hayo yamesemwa na msimamizi wa masuala ya biashara katika mkoa wa Halab nchini Syria kufuatia hatua inayochukua serikali ya Ufaransa dhidi ya waandamanji wa nchi hiyo na kusisitiza kuwa serikali ya Ufaransa inapaswa kuwekewa vikwazo kama inavyowafanyia wananchi wake

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kufuatia maandamano yanayoendelea nchini Ufaransa na maamuzi mabaya yaliochukuliwa na serikali ya nchi hiyo dhidi ya wananchi hao, na kuitaka serikali ya Syria kuiwekea vikwazo serikali ya Ufaransa kama ilivyokuwa ianfanya Ufaransa dhidi ya Syria.
Aidha Faris AS-Shahabiy ambaye ni mkuu wa masoko ya Halab nchini Syria na kusisitiza kile kinachojiri nchini Ufaransa kina fanana yale yaliotokea mnamo mwaka 2011 katika mji wa Halab na kusababisha kuwekewa vikwazo msimamizi wa masoko ya Halab, pamoja yakuwa idadi ya waandamanaji wa Halab haikuwa kubwa kama Paris, hivyo basi ili kuleta uadilifu, msimamizi mkuu wa masoko ya Ufaransa anapaswa kuwekwa katika orodha ya waliowekewa vikwazo.
Kwa mujibu wa ripoti ziliotufikia ni kwamba idadi kubwa ya wafaransa walianza maandamano makubwa manamo 17 ya mwezi wa 11 na kusambaa katika barabara za Paris dhidi ya siasa ya uchumi wa nchini huyo, maandamano ambayo yamekuwa yakiendelea mpaka hivi sasa.

mwisho/290